April 15, 2021




KUTOKA pande mbalimbali, mashabiki wamekuwa wakijitokeza uwanjani kwa ajili ya kutoa sapoti kwa wachezaji wao wanapokuwa uwanjani.

 

Hii inaamanisha kwamba furaha yao ni kuona timu inacheza na kupata matokeo mazuri. Hakuna kingine ambacho mashabiki wanajua zaidi ya kufurahi pale timu inaposhinda.

 

Wengine wamekuwa wakilia pale timu inapopoteza na wengine hata sare pia wanaumia, nina amini kwamba wachezaji wanaona haya ambayo yanatokea wanapaswa wawalipe mashabiki kwa kuwapa matokeo mazuri.

 

Kiujumla ligi imekuwa na ushindani mkubwa, tangu mzunguko wa kwanza na sasa mzunguko  wa pili umeanza kwa kasi kwa kila timu kupambana.


 Wachezaji wamekuwa wakipambana kuonyesha uwezo  uwanja na ni jambo la msingi linalotakiwa kwa kuwa kazi yao ni kucheza na kutafuta matokeo kwenye mechi zote.


Ushindani ndani ya ligi ya msimu huu umechangiwa kwa kiasi kikubwa na usajili ambao umefanyika kwenye kila klabu inayoshiriki msimu huu.


Tayari nina amini kwamba wachezaji ambao walisajiliwa na timu zao mpya na wale ambao wapo kwenye timu ambazo wapo kwa sasa wameshaanza kujenga picha ya kile ambacho wamekifanya. 

 

Na ushindani wa namba umekuwa ni mkubwa kwenye timu zote katika mechi kuanzia zile za kirafiki mpaka za ligi. Kumekuwa na utofauti kila leo kwenye mechi ambazo wachezaji wanacheza.

Kwa namna ambavyo lala salama inakwenda hakuna ambaye yupo salama kwa upande wa zile ambazo zinapambana kushuka daraja na vita ya kuwania ubingwa wa ligi na hii inatokana pia na uwepo wa wachezaji wanaotimiza majukumu yao kwenye timu zao.

Ushindani ule wa kweli unahitajika kwa kuwa ili timu ipate kushinda ni lazima iwe na wachezaji makini na wenye uwezo ambao wanaweza kuipa timu matokeo.

 

Kila wakati ndani ya ligi kunapaswa kuwe na ushindani kuanzia mwanzo mpaka mwisho hii itaongeza thamani ya ligi pamoja na mchezaji mwenyewe ndani ya uwanja

 

Zipo ambazo kwa sasa zimeona mwanga wa kubaki kwenye ligi na nyingine zinaishi kwa hisia kwamba zipo kwenye ligi huku akili zao zikiwa Ligi Daraja la Kwanza 

 

Kilichobaki kwa sasa ni kumaliza hesabu zile ambazo zilikuwa zimepangwa kwa sababu hakuna ambaye anahitaji kuona timu yake ikipoteza mechi ambazo itacheza.


Ikiwa timu zinashuka inaamisha kwamba zipo ambazo zinapanda hivyo hapo kila timu ni lazima iwe na tahadhari katika hatua ambayo itakuwa ipo.


Jambo la msingi kwa wachezaji ni kutimiza majukumu yao wawapo uwanjani. Na kitakachowafanya wapate matokeo nikuzingatia maelekezo ambayo wanapewa na benchi la ufundi.


Kupitia yale maelekezo inaamaanisha kwamba itawapa mwanga wachezaji kujua kinachowapasa wafanye bila kuchoka katika kusaka ushindi. 

Pia ni muhimu kwa wachezaji kuwa na nidhamu katika kutimiza majukumu yao. Nidhamu ni muhimu kwa kila mchezaji iwe ni nje ya uwanja na ndani ya uwanja katika harakati za kusaka ushindi.


Pia ninapenda pia kupongeza kuhusiana na mwamko mkubwa wa mashabiki wa soka hapa nchini ambao wamekuwa wakizidi kuwa na mapenzi makubwa na mchezo wa soka kila kukicha.

 

Ni muhimu hamasa hizi zikaendelea kuongezeka kwani kwa kufanya hivyo mashabiki wengi zaidi watahamasika kujitokeza uwanjani kuzishuhudia timu zao ambapo kiujumla mapato yatakayopatikana kupitia viingilio vyao yanaweza kuzisaidia timu zao kujiendesha kiuchumi.

Lakini pia viongozi wa mashabiki kwenye matawi mbalimbali hapa nchini wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuwahamasisha wenzao ili kusapoti miradi mbalimbali ya klabu kama vile ununuaji wa jezi orijino za klabu zao.

 

Pia nawapongeza Azam Tv ambao wamekuwa wakirusha matangazo ya michezo moja kwa moja yaani 'mubashara'.

  

Kupitia matangazo hayo si tu kwamba Watanzania ambao hawana nafasi ya kuingia uwanjani nao wanapata burudani kupitia matangazo ya televisheni lakini pia wapenzi wa soka wanapata nafasi ya kujifunza.

 

 Sio Tanzania pekee bali hata Zambia, Afrika Kusini nimekuwa nikiulizwa na marafiki zangu kuhusu mwendo wa ligi na namna ambavyo wanashuhudia kazi inavyokwenda.


Hii ni fursa kwa wachezaji kuweza kuwa sokoni kwa sababu mawakala wengi wanafuatilia ligi na kuona namna gani wanaweza kupata wachezaji kwa ajili ya kuwauza.

 

Wakati huu wa lala salama bado wachezaji hamjachelewa mna kazi ya kutimiza majukumu yenu kwa wakati na itawafanya muweze kupata nafasi nje ya nchi na sio Tanzania pekee.

 

 

 

 

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic