April 15, 2021

 NYOTA wa Simba Clatous Chama ameweka rekodi ya kuwa namba moja kwa wanatengeneza pasi za mwisho ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21.

Ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar,  Uwanja wa Mkapa wakati Simba ikifikisha jumla ya pointi 49 Chama amefikisha pasi 10.

Mbali na kuwa na pasi 10 ana mabao pia nyota huyo ametupia jumla ya mabao 7 kwa msimu huu akiwa ni moja ya viungo bora wanaofanya vizuri ndani ya ligi.


Anayemfuata kwa kuwa na pasi nyingi za mwisho ni mshikaji wake Luis Miquissone ambaye naye anacheza ndani ya Simba akiwa na pasi 9 za mabao.


Wote hawa ni wageni ambao wanafanya vizuri jambo ambalo linatoa somo kwa wazawa kupambana kufanya vizuri.


Ni David Luhende wa Kagera Sugar beki mzawa ambaye ana pasi nyingi za mabao akiwa nazo 7 pia ana bao moja.


Ila Luis yeye ni raia wa Msumbiji na Chama ni Mwamba wa Lusaka raia wa Zambia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic