April 9, 2021


MSHAMBULIAJI wa kikosi cha Al Ahly ya Misri, Walter Bwalya kuna hatihati akawakosa Simba leo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika,  hatua ya makundi.

Bwalya alikuwa sehemu ya kikosi kilichoanza Uwanja wa Mkapa wakati ubao ukisoma Simba 1-0 Al Ahly ambapo bao la ushindi lilifungwa na kiungo Luis Miquissone.

Bwalya aliwekwa kwenye ulinzi wa mchezaji bora chaguo la mashabiki kwa mwezi Machi Joash Onyango jambo lililomfanya ashindwe kufurukuta licha ya kufanya majaribio kadhaa ambayo hayakuwa na hatari mbele ya Aishi Manula. 

Mbali na Bwalya ambaye hayupo fiti kutokana na kusumbuliwa na majeraha pia Hamdy Fathy na Ali Maalod watakosekana kwa kuwa wanatibu majeraha.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki, leo Aprili 9.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic