April 15, 2021


JUMA Mwambusi, Kaimu Kocha wa Yanga amesema kuwa ataanza kuboresha safu ya ulinzi ili isifanye makosa ya kuruhusu mabao kwenye mechi zote za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

Ukuta wa Yanga unaoongozwa na nahodha, Lamine Moro pamoja na Bakari Mwamnyeto umeruhusu jumla ya mabao 15 baada ya kucheza mechi 24 na mechi dhidi ya Kagera Sugar kwenye sare ya kufungana mabao 3-3 unashikilia rekodi ya kuwa ni mabao mengi kwa msimu huu.

Akizungumza na Championi Jumatano, Mwambusi alisema kuwa safu ya ulinzi inahitaji mabadiliko ili kuwa bora jambo ambalo linamfanya awe anabadilisha pacha itakayoanza kulinda lango.

Wakati ubao ukisoma Yanga 1-1 KMC, Uwanja wa Mkapa Mwambusi alianza na Lamine pamoja na Abdalah Shaibu, “Ninja’ kwenye upande wa mabeki wa kati.

Mwambusi alisema:”Tunajaribu kufanya mabadiliko sanasana ni kuweza kufanya marekebisho kwenye eneo la ulinzi wakati mwingine unaona tunaanza na Juma Makapu na Lamine, awali ilikuwa ni Mwamnyeto, (Bakari) na Lamine na Ninja na Lamine, na unaona kwamba haturuhusu mabao mengi .

“Tumeona makosa ambayo yanatufanya tuwe tunaruhusu mabao, tumejua kwamba ni namna ambavyo wachezaji wanajipanga hivyo bado tupo kwenye maboresho,” alisema Mwambusi.

 

3 COMMENTS:

  1. Hii rap yako itajirudia, sioni kitu

    ReplyDelete
  2. Hawajui tatizo lao ni lipi

    ReplyDelete
  3. Kameni sawa Mnyama anakungojeeni msije mkalia maonevo na huku mnamuona Mnyama anavonguruma kila kona akiilaža miamba ya Africa bila ya huruma

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic