April 15, 2021


RIO Ferdinand beki wa zamani wa Manchester United na mchambuzi wa masuala ya michezo amesema kuwa bado anajiuliza kuhusu anguko la Klabu ya Liverpool kwa msimu huu chini ya Kocha Mkuu, Jurggen Klopp.

Liverpool imekuwa kwenye mwendo wa kusuasua msimu huu baada ya msimu uliopita kuwa bora na iliweza kutwaa taji la Ligi Kuu England ambalo kwa sasa inaonekana wazi kwamba inalipoteza kwa kuwa ipo nafasi ya sita na pointi zake 52 vinara wakiwa ni Manchester City na pointi zao ni 74.

Klopp ameondolewa kwenye Champions League na Real Madrid baada ya kushindwa kupindua meza kwenye robo fainali ya pili pale Uwanja wa Anfield ubao uliposoma Liverpool 0-0 Real Madrid, mchezo wa kwanza walipoteza kwa kufungwa mabao 3-1 ugenini.

Beki huyo amesema kuwa bado haelewi ambacho kinaisumbua Liverpool kwa sasa anadhani labda wachezaji wamekuwa wakicheza chini ya kiwango ama majeruhi yanaitesa timu hiyo kwa sasa.

"Kuna maswali ambayo tumekuwa tukijiuliza kwamba kwa nini Liverpool imekuwa inafanya namna hii, labda inaweza kuwa sababu ya aina ya mbinu za mwalimu Klopp? Amekuwa na timu kwa miaka minne , mitano hivi hivyo anawajua wachezaji wake.

"Labda kuna mambo ambayo hayapo sawa itakuwa ni msimu mbaya tu ama kukosa wachezaji wake muhimu kikosini kwa kusumbuliwa na majeraha? 

Kwa sasa Liverpool yenye mshambuliaji Mohamed Salah inapeleka nguvu kwenye Ligi Kuu England ili kutetea taji lao.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic