ZLATAN Ibrahimovic, staa wa Klabu ya AC Milan anatarajiwa kuongeza mkataba wa mwaka mmoja ndani ya Klabu hiyo ambapo atakuwa akilipwa pauni 5.94m kwa mwaka.
Nyota huyo mwenye miaka 39 mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
Kuanzia sasa Zlatan anatarajiwa kusaini mkataba mpya ndani ya timu hiyo inayoshiriki Serie A.
Msimu huu kwenye Serie A ametupia jumla ya mabao 15 kati ya 54 ambayo yamefungwa na timu yake baada ya kucheza jumla ya mechi 29.
Kinara wa Serie A ni Inter Milan akiwa na pointi 71 huku AC Milan ikiwa nafasi ya pili na pointi 60.
0 COMMENTS:
Post a Comment