NDANI ya Ligi Kuu Bara Tanzania, kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula amekaa langoni kwenye jumla ya mechi 22 kati ya 25 ambazo wamecheza na kukusanya pointi 61.
Ikiwa imefungwa jumla ya mabao 10, Manula ameokota nyavuni jumla ya mabao 9 katika mechi 8 ambazo alifungwa huku akikusanya jumla ya clean sheet 14.
Ni mechi 22 ambazo amekaa langoni huku mechi mbili pekee akifanyiwa mabadiliko ilikuwa mbele ya KMC alipotumia dakika 45 na mbele ya JKT Tanzania alitumia dakika 67.
Jumla ametumia dakika 1912 na ana wastani wa kuokota bao moja nyavuni kila baada ya dakika 212.








jitahidi hivyo mdogo wangu kweli nikikuanglia sasa na nikikumbuka hapo mwanzo kweli umebadilika kwa kiasi kikubwa mdogo wangu kila la kheri dogo ila usibweteke na sifa wewe endelea kudaka mpira kama nyani
ReplyDeleteMami namuusia abaki hapo Simba Kwani wa kale walisema "usiwache mbachao kwa msala upitao" kwani umashuhuri huo umeupatia hapo na huna hakika nako huko unapotakiwa nyota yako ipo Simba, wengi waliondoka na haukupita muda na wakasahaulikana kabisa na kurejea nyumbani na kusahauliwa wakijificha katika vitimu bila kuonekana au hata kusikia
ReplyDelete