May 30, 2021

 


BAADA ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza majeraha ya mguu, Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Balama Mapinduzi, kesho Jumatatu anatarajiwa kuanza mazoezi maalum ya uwanjani.

 

Balama alivunjika mguu akiwa mazoezini katika maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara msimu uliopita ambapo hadi sasa hajaonekana uwanjani.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema: “Kwa mujibu wa daktari, tayari Balama amepona na anatarajiwa kuanza mazoezi Jumatatu timu ikirejea kambini.

 

“Alikuwa nje kwa muda mrefu, hivyo atakaporejea daktari na benchi la ufundi watakaa na kuona watampa mazoezi yake binafsi.

 

Kwa upande wa wachezaji wengine ambao walikuwa majeruhi, dokta atatoa ripoti watakaporejea kambini Jumatatu.”Mbali na Balama, nyota wengine wa Yanga ambao ni majeruhi ni Saidi Ntibazonkiza, Carlos Carlinhos na Abdallah Shaibu ‘Ninja’

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic