May 1, 2021


 CLATOUS Chama, kiungo mshambuliaji wa Simba raia wa Zambia rekodi zinaonyesha kuwa akiwa amehusika kwenye mabao 20 kati ya 58 yaliyofungwa na timu hiyo ana wastani wa kuwa na hatari kila baada ya dakika 88.

Chama ametupia mabao 7 na kutoa pasi 13 akiwa ni namba moja kwa watengeneza pasi za mwisho pia amevunja rekodi yake ya msimu uliopita wa 2019/20 ambapo alifunga mabao mawili na kutoa pasi 10.

Msimu huu amecheza mechi 22 kati ya 25 amefunga mabao 7, ametumia dakika 1,764 akiwa anapewa nafasi ya kuweza kutetea tuzo yake ya mchezaji bora wa ligi msimu uliopita.

Pia anapewa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Yanga ambao ni wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Mei 8, Uwanja wa Mkapa.

 Mechi zake msimu huu ambazo aliyeyusha  dakika 90 ilikuwa mbele ya :-Ihefu, Mtibwa Sugar, Biashara United, Mwadui FC, Yanga, Coastal Union, Mbeya City, KMC,  Ihefu, Azam FC , JKT Tanzania, Mtibwa Sugar , Mwadui , Kagera Sugar , Gwambina FC na Dodoma Jiji.

Nyingine ilikuwa namna hii ambapo hakuyeyusha dakika zote 90:-Gwambina dk, 86, JKT Tanzania, 77, Kagera Sugar, 68, Polisi Tanzania, dk 29, Biashara United, dk 31 na Prisons, 33.

Gomes ameliambia Spoti Xtra kuwa wachezaji wake wote ni bora jambo ambalo linampa furaha pale wanapotimiza majukumu yao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic