May 29, 2021


IMEELEZWA kuwa nyota wa kikosi cha Juventus, Cristiano Ronaldo ameshawajulisha wachezaji wenzake wa kikosi hicho kuwa anataka kuondoka baada ya msimu huu kumeguka.

Ronaldo alijunga na Juventus mwaka 2018 akitokea Real Madrid ila msimu huu timu yake imekwama kutwaa taji la Serie A pamoja na taji la Ulaya jambo ambalo linaongeza nafasi kwa nyota huyo kuondoka.

Mkataba wake kwa sasa ndani ya timu hiyo bado umesalia mwaka mmoja ila inaelezwa kuwa anahitaji kuondoka pale dirisha la usajili litakapofunguliwa.

Miongoni mwa timu ambazo zinatajwa kuwania saini yake ni pamoja na Manchester United na Sporting CP pia Real Madrid walikuwa wanatajwa ila wamekanusha kwamba hawahitaji saini yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic