May 29, 2021


RAHEEM Sterling nyota wa kikosi cha Manchester City huenda akauzwa msimu huu utakapoisha kwa kuwa anatajwa kwamba hayupo kwenye hesabu za Kocha Mkuu, Pep Guardiola.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu England leo wana kazi ya kucheza mbele ya Chelsea kwenye mchezo wa fainali ya Champions League utakaochezwa Porto majira ya saa nne usiku.

Sterling mwenye miaka 26 amepoteza nafasi yake kikosi cha kwanza hivi karibuni hivyo City wanasubiri kama wanaweza kupata ofa inayomuhitaji mchezaji huyo.

Sio yeye peke yake ambaye anaweza kusepa pia yupo nyota mwingine Riyad Mahrez ambaye naye ni miongoni mwa wale ambao wataondoka City na timu ambayo inapewa nafasi ya kuwachukua nyota hao wawili ni Arsenal.


Kwa sasa Arsenal inayonolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta inapewa nafasi ya kuwasajili wachezaji hao kwa sababu Arteta aliwahi kufanya kazi na vijana hao zama zile alipokuwa ndani ya City akiwa ni kocha msaidizi.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic