SHIRIKISHO la Soka la Ulaya (UEFA) limethibitisha kuwa Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu kati ya Chelsea na Manchester City itapigwa katika Uwanja wa Dragao, jijini Porto, Ureno Mei 29, mwaka huu.
Fainali hizo kwa sasa zitapigwa katika uwanja huo ambao hutumiwa na Klabu ya FC Porto na wataruhusiwa mashabiki 6000 kuingia na uwanja unawezo wa kubeba mashabiki 50,035.
Awali fainali hizo zilipagwa kufanyika Istanbul, Uturuki katika Uwanja wa Ataturk ila ilishindikana kutokana na masuala ya janga la virusi vya Corona. Kwa maana hiyo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya pili mfululizo itapigwa ndani ya Ureno.
Msimu uliopita fainali ilichezwa katika Uwanja wa Da Luz, Lisbon wakati Bayern Munich ikitwaa ubingwa dhidi ya Paris Saint Germain. Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin alisema:
“Kwa mara nyingine tumerudi kwa rafi ki zetu Ureno wametusaidia shukrani kwa chama cha soka cha Ureno pamoja na Serikali kuweza kutupa nafasi tena kwa muda mfupi tu kwa kulifanikisha hili.
“Tulipitia vikwazo vingi, lakini tumefanikiwa kumaliza hilo, baaada ya mwaka sasa mashabiki watafanikiwa kuangalia timu zao zikicheza katika fainali ya UEFA safari hii.”
0 COMMENTS:
Post a Comment