IMERIPOTIWA kuwa mabosi wa Klabu ya Barcelona wanamfuatilia kwa ukaribu nyota wa Borussia Dortmund, Erling Haaland ili kupata saini yake.
Barcelona wanahitaji kupata saini ya Haaland mwenye miaka 20 ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya kumlinda nyota wao Lionel Messi ili abaki msimu ujao kwa kuwa imekuwa inaripotiwa kwamba anahitaji kuondoka.
Kwa kufanya hivyo Barcelona itakuwa imeingia kwenye vita na wapinzani wao ndani ya La Liga ambao ni Real Madrid na timu nyingine ambazo zinashiriki Ligi Kuu England ambazo ni pamoja na Manchester United, Manchester City, Chelsea na Mancheter City zinazoripotiwa kuhitaji saini yake.
Mshambuliaji huyo amekuwa na rekodi bora ambapo amefunga jumla ya mabao 55 katika jumla ya mechi 57 ambazo amecheza jambo ambalo linafanya thamani yake izidi kuwa kubwa ambapo imeripotiwa kwamba mabosi wake wa sasa wa Dortmund wamesema kuwa kuipata saini ya nyota huyo sio chini ya euro milioni 154.
0 COMMENTS:
Post a Comment