BENCHI la ufundi la timu ya AS Vita ya DR
Congo limebariki rasmi beki wa pembeni wa
timu hiyo, Djuma Shabaan kujiunga na Yanga
ikiwa tu watafikia kwenye makubaliano mazuri.
Beki huyo wa kimataifa wa DR Congo amekuwa
katika kiwango bora, kiasi ambacho amezivutia
timu nyingi ikiwemo Yanga ambayo inaelezwa
wapo katika hatua nzuri ya kuweza kumnasa
beki huyo ambaye amehusishwa na kutakiwa
na Simba hivi karibuni.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Kocha
Msaidizi wa AS Vita, Raoul Shungu, amefichua
kuwa kwa upande wao hawawezi kumzuia
mchezaji yeyote kuondoka kwenye timu hiyo
ikiwa atapewa maslahi mazuri, hivyo kama
Yanga watatoa fedha watampata na litakuwa
jambo zuri kwa mchezaji huyo.
“Kuhusu unachoniambia kwa
upande wetu wala hatuna tatizo kama benchi la
ufundi tupo tayari kumuachia.
“Unajua kwa upande wetu ligi ikishamalizika,
tunatoa ruhusa kwa mchezaji yeyote kuondoka,
sasa suala la Djuma ni hao Yanga wenyewe
kufikia makubaliano na mchezaji ili aweze kujiunga nao, sisi hatuna shida kwa kuwa tuna
kawaida ya kutengeneza wengine,” alisema.
Wanataka kyingilia dili ya simba ili kumpandisha vei, utopolo bwana? Hii A.S Vita nayo ni kama tawi la utopolo tuu, mara shungu, mara ibenge, mara yule jamaa aliyekuwa gwambina ili mradi wote wanavinasaba vya utopolo
ReplyDeleteHa ha ha ha ha ha acha kuweweseka dude,mpira pesa bhana ,alafu future na goals za mchezaji anazijua mwenyewe,kwahyo wewe hata ukiongea haisaidii chochote,inawezekana future yake ilikua kucheza yanga hatakama haishiriki michuano mikubwa,alafu Simba sio watu wakukurupuka brother hivyo inawezekana wametonywa Kwa namna fulan,Kwa Simba hii hakuna mchezaji ndani ya bara letu haswa ukanda huu wa black people's kushindikana kusajiliwa Simba labda tu Simba yenyewe ndio imkatae
ReplyDeleteNguruwe fc mnajikweza sana et kuingilia dili la SIMBA! Lini simba ikawa na ubavu wa kusajili mchezaji mwenye mkataba hasa kutoka nchi kama DRC
ReplyDeleteKwa hiyo hata Morison hakuwa na mkataba eti
DeleteUtopoloooo... Mnajisifia kuvunja mikataba sasa imewasaidia nini
DeleteDjma hawezi kuenda yanga achen kjidandanya kasa sain huko waydad Casablanca
ReplyDeleteUtopolo mpira wao ni mdomoni na kwenye vyombo vya habari Ila uwanjani hakuna kitu
ReplyDelete