May 13, 2021


KIUNGO wa Klabu ya Yanga ambaye ni mkongwe ndani ya Ligi Kuu Bara kwa sasa anapata tabu kupata namba kikosi cha kwanza tofauti na zamani ambapo alikuwa ni chaguo la kwanza.

Nyota huyo pia ameweza kucheza katika timu zote mbili kubwa ambazo ni Simba na Yanga na aliweza kutwaa taji la ligi alipokuwa ndani ya Simba na kikosi hicho kilitinga hatua ya robo fainali.

Msimu huu wa 2020/21 akiwa ndani ya Yanga iliyocheza jumla ya mechi 27 Niyonzima ameweza kucheza jumla ya mechi 12 na kutumia dakika 371.

Tabu anayopata ni kwamba kwenye mechi hizo 12 hajapata bahati ya kuyeyusha dakika zote 90 pia hajafunga bao wala kutengeneza pasi ya bao.

Mechi zake ilikuwa namna hii:-Mbeya City, dk 69, Kagera Sugar, dk 7, Coastal Union, dk 45, Polisi Tanzania, dk 59, KMC 9, Ruvu Shooting, 19, Mwadui dk 30, Ihefu, dk 14, Kagera Sugar, dk 16, Polisi Tanzania, dk 77, Biashara United dk 14, Azam FC, dk  12.

Kuhusu nafasi yake ndani ya kikosi cha Yanga ambacho kinanolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi Niyonzima alisema kuwa anamuachia mwalimu ila kazi yake yeye ni kucheza.

“Mimi ni mchezaji na jukumu la kuanza ama kutoanza hiyo ni kazi ya mwalimu. Nikipata nafasi ninatimiza majukumu yangu kwa ajili ya kuisaidia timu yangu, hivyo kuanza ama kutokuanza hilo lipo mikononi mwa mwalimu,” alisema.

5 COMMENTS:

  1. Wachonganishi acheni upuuzi huu

    ReplyDelete
  2. Kiwango kinatoweka na umri umeanza kuuwacha mkono. yuko wapi Tambwe

    ReplyDelete
    Replies
    1. UKWELI MCHUNGU, HARUNA YUKO YUKO UNDER RATED NOW! NA KINGINE MALINGO MENGI, ANADHANI HISTORIA INACHEZA, WAKATI CHAMA ANAFIKA SIMBA AKASEMA ASILINGANISHWE NA CHAMA, JE LEO ANA CHOCHOTE CHA KULINGANA NAE CHAMA? MABDAILIKO YA WALIMU NA MIFUMO MARA KWA MARA INAMPOTEZA ZAIDI. NASREDEEN NABI ANAPENDA KUJIHAMI KWA HIYO ATAHITAJI WATU WAKABE SANA NA KUSHAMBULIA KIASI, GOLI MOJA LINATOSHA.

      Delete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  4. Acheni Uongo. Niyonzima alifunga mechi na coastal Union Dar es Salaam katika ushindi wa 3- 1

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic