KLABU ya Tottenham ina mpango wa kumuongezea muda wa mkopo kiungo mshambuliaji, Gareth Bale ambaye yupo hapo kwa mkopo akitokea kikosi cha Real Madrid.
Raia huyo wa Wales mkataba wake na Real Madrid unatarajiwa kufika tamati Juni 20, 2022.
Bale amekuwa akiweka wazi kwamba anahitaji kurejea katika timu yake hiyo ili aweze kupata changamoto tena chini ya Kocha Mkuu, Zinedine Zidane kwa kuwa ameshapata uzoefu.
Lengo la nyota huyo ni kwenda kumalizia mkataba wake katika timu yake tofauti na hapo alipo kwa sasa.
Mwenyekiti wa timu hiyo, Daniel Levy anafanya jitihada kuhakikisha kwamba Bale anasalia kikosini hapo msimu wa 2021/22.
0 COMMENTS:
Post a Comment