May 14, 2021

 


WAKATI baadhi ya mastaa wa kikosi cha Yanga wakitarajiwa kumaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu, uongozi wa Yanga umesema kwamba, hatma ya wale ambao wataongezewa mikataba, ipo chini ya kocha wao, Nasreddine Nabi.

 

Baadhi ya wachezaji wa Yanga wanaotarajiwa kumaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu ni Saidi Makapu, Deus Kaseke, Faroukh Shikhalo, Metacha Mnata na Fiston Abdoul Razack.

 

Nabi raia wa Tunisia, amekabidhiwa kikosi hicho Aprili 20, mwaka huu ambapo anatarajiwa kuisuka upya timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao ambapo wana asilimia kubwa ya kushiriki michuano ya kimataifa.


Akizungumza na Spoti Xtra, Mkurugenzi wa Mashindano Yanga, Thabit Kandoro, alisema: “Wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu, suala lao tayari lipo katika kamati ya usajili.

 

“Kwa sasa tunasubiri ripoti ya kocha mkuu kama atawahitaji kwa msimu ujao basi wataongezewa mikataba, hivyo yeye ndiye atakayeamua hatma yao kutokana na viwango vyao mazoezini na kwenye mechi.

 

“Kocha Nabi kwa sasa anaandaa kikosi sio kwa ajili ya michuano ya ndani tu, bali kwa ajili ya michuano ya kimataifa ambayo tunaweza kushiriki msimu ujao.”

2 COMMENTS:

  1. Wachambuzi uchwara wapo kimyaa kuhusu wachezaji wa timu zingine.Ingekuwa Simba kingewaka moto kwenye studio zao za kizandiki.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ina uhusiano gani? Umelewa pilau la sikukuu

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic