MABOSI wa Yanga imeelezwa kuwa kwa sasa wamefikia maamuzi mazuri na beki wa kati ambaye ni nahodha Mghana, Lamine Moro na kumrejesha kikosini.
Hiyo ikiwa ni siku chache tangu beki huyo
aondolewe kwenye kikosi cha timu hiyo na
Kocha Mkuu wa Yanga raia wa Tunisia,
Nasreddine Nabi kwa kile kilichoelezwa utovu
wa nidhamu.
Beki huyo aliondolewa akiwa Ruangwa, Lindi
wakati timu hiyo ilipokwenda kucheza mchezo
wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC kwenye
Uwanja wa Kassim Majaliwa.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Mkuu wa
Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa timu
hiyo, Hassan Bumbuli, alisema kuwa uongozi
wa Yanga umefikia muafaka mzuri na beki wake
baada ya wiki iliyopita kukaa naye kikao na
kusikiliza madai yake.
Bumbuli alisema kuwa uongozi ulifanya kikao
na beki huyo kwa ajili ya kusikiliza utetezi wake
kutokana na kosa alilolitenda ambalo
limefichwa, kabla ya kumsamehe.
Aliongeza kuwa, tofauti hizo mbili kati ya kocha
na Lamine wamezimaliza na beki huyo
atajiunga na timu mara baada ya kurejea juzi
Jumatano jijini Dar wakitokea kucheza mchezo
wa robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Mwadui
ambao ulimalizika kwa Yanga kushinda mabao
2-0.
“Isingekuwa vizuri uongozi kuchukua maamuzi
ya kumuondoa kabisa kikosini Lamine bila ya
kumsikiliza yeye, hivyo uongozi wiki iliyopita ulimuita na kufanya naye kikao kwa lengo la kusikiliza utetezi wake.
“Hiyo ni baada ya tatizo hilo kutokea kambini ambako hawakuwepo viongozi, hivyo tulimsikiliza kocha na wiki iliyopita tulimsikiliza Lamine utetezi wake, hivyo suala hilo tumelimaliza salama,” alisema Bumbuli.
“Baada ya kumaliza tatizo hilo, uongozi ulimbakisha hapa Dar kutokana na kutokuwepo katika mipango ya kocha kuelekea mchezo wetu wa FA dhidi ya Mwadui FC tuliocheza Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.”
Wenye kosa ni wao, anawadai hela kwa nini wampakazie masuala ya nidhamu?
ReplyDeleteMambo hayo wameitwa wote wawili wajieleze ili ajulikane nani makosa baina ya kocha na mchezaji ikiwa ni hivo si itakuwa kusutana baina ya wawili hao tena lazima Mmoja atakuwa makosa ikiwa ni hivo nini tutaraji kuhusu disiplini ya kikosi, tunajenga au kubomoa
ReplyDeleteWachezeji siyo wakubwa kuliko Coaches wala Clubs. Wakikosa waadhibiwe period
ReplyDelete