May 1, 2021


BAADA ya nahodha wa Tanzania Prisons, Benjamin Asukile kuweka wazi kuwa walizidiwa kwa kuwa refa hakuwa upande wao, Ofisa Habari wa Yanga amemtaka nahodha huyo aweze kuthibitisha suala hilo.

Jana, Uwanja wa Nelson Mandela kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho, hatua ya 16 bora, ubao ulisoma Prisons 0-1 Yanga na kuwafanya Yanga watinge hatua ya robo fainali.

Asukile aliweka wazi kwamba walishindwa mchezo huo kwa kuwa mwamuzi hakuwa upande wao huku akisema kuwa bao ambalo walifungwa na Yacouba Songne lilikuwa halali.

Kupitia Ukurasa rasmi wa Istagram wa Hassan Bumbuli ameandika namna hii:-" Nahodha wa Tanzania Prisons Benjamin Asukile ametoa tuhuma nzito dhidi ya Yanga, 1. Amesema tuliwazidi kwa sababu tulimuongeza Refa upande wetu, Hili tunataka alithibitishe, Kivipi na kwa namna gani!?

2. Walikuwa wakiwapigia simu na kutaka kutoa Mil 40 (Rushwa) Ili watuachie game, hili pia tunataka alithibishe mbele ya ya Mamlaka husika.

Hakuna namna ambayo Yanga tunaweza kuvumilia kuchafuliwa kwa kiwango hiki. Asukile anasahahu kwamba ushindi pekee ambao timu yake imewahi kuupata tangu msimu wa 2018/19 hadi sasa ni sare tatu tu katika mechi nane.

Msimu wa 2018/19 tuliwafunga mabao 3-1 kwao, pia tukawafunga 2-1 kwa Mkapa. Msimu wa 2019/20 tuliwafunga 1-0 kwao (Samora), wakaambulia sare kwa Mkapa na tukawatoa kwenye FA kwa mabao 2-0.

Msimu huu wamebahatika kupata sare mechi zote mbili za ligi, na jana wamekaa kwao, sasa huo ujasili wa Asukile na kujitoa ufahamu kuona wao ni wababe ameutoa wapi? Tutazifikisha tuhuma hizi zote kwa mamlaka husika ASAP.

13 COMMENTS:

  1. Kuwafunga mechi zilizopita sio kigezo cha kuwafunga mechi zote, na Wala asukile hajasema kuwa niwababe kuliko nyie. Cha msingi asukile apewe nafasi ili atoe ushahidi Wala hakuna haja ya kutoa povu jiiiiingi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na alushindwa kutoa ushahidi achukuliwe hatua za kisheria.

      Delete
  2. Hapo ndio tunapopataka, mashauri yafunguliwe tuone nani msema kweli, tumeanza kuona dalili za kuhonga wazi wazi

    ReplyDelete
  3. Kama walishindwana na timu kuhusu hyo mil 40 basi yaweza kuwa walimalizana na refa mwenyew coz hata blocking ya wazi kwa mchezaj aliyetaka kuifunga utopol ni ya wazi but kocha akauma kipyenga..ila kama kuna ukweli basi ujanjaujanja haumfikishi mtu mbali bali kuwa mjanja ndo jambo zuri..tutaona next step..

    ReplyDelete
  4. Yanga wanapenda sana historia. Yaani unataka kuhalalisha ushindi wa sasa kwa kuwa zamani uliwashinda pia? Mbona sasa maana ya soka kuwa na matokeo matatu inapotea? Timu yoyote inaweza ikapata matokeo yoyote katika mechi tofauti kutegemeana na maandalizi na hali ya wapinzani wako kwa sasa, na sio kwa wakati uliopita. Hii hoja ya kihistoria ni nyepesi mno kufuta madai ya Asukile

    ReplyDelete
  5. Kwani paka fc mbona kama wanateseka yanga inapofanya vzr? Yanga ni wakubwa zenu bhana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Utopolo bhana hawanaga hoja za msingi

      Delete
  6. Hii kweli Simba mnatisha,mmetuzungusha mnaandaa matimu yacheze na Yanga kibabe,mnaongoza kwa rushwa ni Simba hii tu ya ratiba tu ni rushwa tosha ukiangalia kwa macho .

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unachosema ni kweli na ili jamaa aendelee kuwepo na kuwafyonza lazima apenyeze tukamiwe

      Delete
  7. Nguruwe pori wenu hatujamskia vipi yuko wapi

    ReplyDelete
  8. Wanasimba mtaugua mishipa msipoacha maisha ya uswahili ,Timu zinapocheza na ninyi hawakamii hata body contact zinakuwa chache wanawaacha mcheze mnavyotaka,ukiangalia wengine wanajiangusha ili mchezaji wenu apite yote tunaona tunacheeeeeka

    ReplyDelete
  9. Yaani huyo asukile kweli.....kikwetu amesuka....ametoa povu inawezekana mikia walihonga ili tusiwafunge

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic