MOHAMED Abdalah, 'Bares' , Kocha Mkuu wa JKT Tanzania amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya mechi zao zilizobaki ili kupata matokeo chanya.
JKT Tanzania imetoka kusepa na pointi tatu mbele ya Gwambina FC kwa ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Gwambina Complex.
Mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Yanga unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, Mei 19.
Akizungumza na Saleh Jembe, Bares amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zao zilizobaki na wanaamini kwamba watapata matokeo.
"Tupo tayari kwa ajili ya mechi zetu zijazo na tunaamini kwamba tutapata matokeo chanya kikubwa ni kila mchezaji kutimiza majukumu yake," .
0 COMMENTS:
Post a Comment