May 17, 2021

KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu Didier Gomes leo Mei 17 kimewasili salama Tanzania kikitokea nchi Afrika Kusini.

Kimeongonzana na viongozi wake ikiwa ni pamoja na Crestius Magori ambaye alikuwa kwenye msafara huo, Haji Manara, Ofisa Habari wa Simba, Patrick Rweyemamu, meneja wa Simba.

Kikosi hicho kilikuwa Afrika Kusini ambapo kilipoteza kwa kufungwa mabao 4-0 dhidi ya Kaizer Chiefs, Uwanja wa FNB Soccer City hivyo kimerejea kwa ajili ya maandalizi ya robo fainali ya pili ya marudio katika Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Mei 22, Uwanja wa Mkapa ambapo Simba ina mlima wa kusaka ushindi wa mabao zaidi ya manne ili kusonga hatua ya nusu fainali.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mratibu wa Simba, Abbas Ally amesema kuwa wanatambua wana kazi kubwa ya kufanya kwa kuwa wamerudi watajipanga kwa ajili ya mchezo huo.

"Tumerudi salama tunajua kwamba tuna mlima mkubwa lakini kwenye soka kila kitu kinawezekana na tutapambana kupata matokeo,".

3 COMMENTS:

  1. ili simba washinde itabidi wacheze mpira wa speed na kushambulia moja kwa moja ili mabeki wa kaizer wafanye makosa na kupata kadi nyingi za njano ziwaogopeshe kuingia kwa nguvu na kusababisha red card na kama ikatokea wakasababisha red card basi kuna uwezekano wa kupata goli nne mechi ikawa droo na lolote baadae linawezekana kutokea na simba ikashinda

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahahahahahahah!!!!!!Hesabu za kufikirika mwisho wake kichwa kitakuuma.Kwa ligi yetu ya Bongo hayo unayofikiri yanawezekana maana ikiwa kama kona ina offiside basi hata red card kwa mchezaji anayekusudiwa kutolewa nje atatolewa bila kujali amefanya kosa au la.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic