BAADA ya kipigo ilichopata Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Mohammed Dewji Mei 16, 2021 aliamua kuwekeza fedha zaidi katika kuitengeneza Simba iweze kushindana zaidi.
Kikosi cha Simba leo Mei 17 kinatarajiwa kurejea Tanzania kikitokea nchini Afrika Kusini ambapo kilipoteza mchezo wake wa kwanza wa robo fainali kwa kukubali ubao usome Kaizer Chiefs 4-0 Simba.
Kupitia Twiter Mo aliandika:-“Nilipanga kujizawadia Ferrari na Rolls-Royce, sina budi kuweka mpango huu kapuni kwa sasa na kuelekeza fedha zaidi katika klabu yetu ya Simba SC Tanzania.
" Furaha ya Simba SC Tanzania ni muhimu kuliko starehe yangu. Simba kwanza!”.
Mchezo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa Mei 22, Uwanja wa Mkapa.
Kwa mkapa aj kutoka mtu
ReplyDeleteVilabu vyetu vyoote hapa are the same shit tunajua kuchonga midomo tu lakini kazi hatuiwezi sio Simba wala Yanga ligi yetu mavi matupu bado tuna siasa za mpira mpaka leo uwongo mwingii vilabu vyetu bado sana kushindana kimataifa tokeni zenu hapa munatutia hasira tu nyinyi wapumbavu kuanzia tff mpaka viongozi wa vilabu kwendeni zenu huko waongo wakubwa nyinyi
ReplyDeletePunguza hasira kaka,toa mawazo chanya wahusika waboreshe penye mapungufu
DeleteTANZANIA hakuna FOOTBALL aiseee ila tunaaminishana tu
ReplyDeleteUnamuona namna ya kiongozi huyo namna anavoipenda naa kuitunza timu yake kufikia hadi kujinyima lakini hela badala ya kununulia alichokipenda akaamuwa kutumia kwa maslahi ya Simba, huyo ndio kiongozi wa kweli
ReplyDeletewewe unaamini hayo, unaona this is what is killing us
ReplyDeletetunaanda timu ili ifike robo fainali au nusu fainali na sio kuchukua kombe na mashabiki wa timu husika hufurahia timu yao inapofikia hatua hizo sasa ndio nini
ReplyDeleteUnakata tamaa mapema...wewe ni utopolo
DeleteTukiondoa uozo TFF huenda vilabu vyetu vikakaa sawa vinginevyo tuendelee na porojo na ngonjera
ReplyDelete