KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mapinduzi Balama anatarajiwa kuanza mazoezi ya pamoja na wenzake hivi karibuni ikiwa ni program maalumu ambayo amepewa.
Nyota huyo aliumia enka Juni, 2020 na kwa sasa anaendelea na matibabu ili kurejea kwenye ubora wake.
Msimu huu hajacheza mchezo hata mmoja wa mashindano ndani ya ardhi ya Bongo kwa sababu ya kutibu enka.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kwa sasa tayari ameshapona na anatembea bila usaidizi wa magongo.
"Kuhusu Balama kwa sasa anaendelea vizuri na amepona kwa kuwa anatembea bila ya usaidizi wa magongo. Anatarajiwa kuungana na wachezaji wenzake ikiwa ni program maalumu ambayo amepewa," .
Chanzo: Championi.
0 COMMENTS:
Post a Comment