Kurejea kwao kambini itakuwa ni kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya mchezo mwingine wa ligi ambao ni dhidi ya Dododma Jiji.
Taarifa rasmi kutoka kitengo cha habari cha KMC, kinachosimamiwa na Christina Mwangala imeeleza kuwa mapumziko hayo yametokana na KMC FC kutokuwa na mchezo wowote wa mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa muda wa mwezi mmoja.
Kwa mujibu wa ratiba ya Bondi ya Ligi Tanzania, (TPLB) mchezo wao unaofuata wa ligi ni Juni 17 itakuwa dhidi ya Dodoa Jiji.
Aidha kufuatia mapumziko hayo, Kocha Mkuu John Simkoko pamoja na msaidizi wake Habibu Kondo wataweka utaratibu wa kufanya mazoezi pindi wachezaji watakaporejea kambini sambamba na kucheza mechi nyingi za kirafiki kwa lengo la kuendelea kujiimarisha na hivyo kufanya vizuri kwenye michezo iliyobakia.
“Tumetoka kupoteza mchezo muhimu dhidi ya Azam FC , lakini bado haitukatishi tamaa kuendelea kupambania nafasi ya nne, hivyo mapumziko haya ni maalumu kwa wachezaji wetu.
"Tukirudi kama timu uongozi kwa ujumla tutaendelea kuweka nguvu zaidi kwenye michezo yetu iliyobaki na hivyo kufanya vizuri ili mwisho wa siku tufikie malengo ambayo tumejiwekea," .
KMC FC imecheza michezo 29 na kufikisha alama 41 ipo nafasi ya tano na imebakiwa na mechi tano mkononikukamilisha msimu wa 2020/2021, ambayo ni dhidi ya Dodoma Jiji, Mtibwa Sugar, JKT Tanzana , Simba pamoja na Ihefu.
0 COMMENTS:
Post a Comment