May 18, 2021


 KIKOSI cha Yanga leo Mei 18 kimewasili salama makao makuu ya Tanzania, Dodoma na kupata fursa ya kuingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kuna vikao vya Bunge ambavyo vinaendelea.

Yanga ilianza safari leo Mei 18 asubuhi kuibukia Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania, unaoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, kesho Mei 19 majira ya saa 10:00 jioni.



Kupitia ukurasa wao rasmi wa Isntagram, Yanga waliandika namna hii:"Timu ya mabingwa wa kihistoria ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,". 

9 COMMENTS:

  1. Hawataki kuiheshimu serikali sijui pale wameenda kufanya nini

    ReplyDelete
  2. Inashangaza wameingia hapo kwa lipi, bora hata ihefu angetinga kuonyesha kuwa alipanda daraja na bado anapambana, hawa wakimbia mechi na kukaidi maagizo ya serikali humo wamefuata nini?

    ReplyDelete
  3. Timu inakimbia uwanjani kisha inaenda Bungeni,hata wao wenyewe ukiwauliza wameenda kufanya nini hawatokuwa na jibu la maana..Tunabaki tukishangaa sisi na wao!

    ReplyDelete
  4. Labda wanaenda kuonyesha kombe la mapinduzi na ubingwa hewa wa kihistoria

    ReplyDelete
  5. Wamekwenda ili wapate huruma za bunge. lakini juu ya hivo ilitakikana iwe Wamekwenda kwakutokana na mwenendo mzuri wa timu yao lakini hilo hakuna.Ati kwakuwa hapo zamani walikuwa mabingwa na walihisi ingelra hamasa lakini hilo halijatokea na walijizuzuwa tu bila ya faida

    ReplyDelete
  6. Kwakuwa wao Wananchi hahaaaa

    ReplyDelete
  7. Wabunge wana kazi zao za kupekeja nchi wanajipeleka kuwatafiri kwa kufikiria wanapenda sana. Wangeouuzwa. Wangefanikuwa kama akuvifanikiwa Mnyama wangetaja kulala hukohuko

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic