May 18, 2021

 


BADRU Mohamed Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar tayari ameanza kazi ya kukinoa kikosi hicho kinachoshiriki Ligi Kuu Bara.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 15 ikiwa imekusanya jumla ya pointi 31 baada ya kucheza jumla ya mechi 29.

Badru ametambulishwa rasmi ndani ya Gwambina jana Mei 17 akitokea Klabu ya Gwambina FC.

Ameiacha Gwambina FC ikiwa nafasi ya 17 baada ya kucheza jumla ya mechi 28 lakini hakuanza msimu na timu hiyo ambayo imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu.

Mchezo wake wa mwisho ilikuwa ni mbele ya JKT Tanzania, Uwanja wa Gwambina Complex na timu yake ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic