KATIKA kuhakikisha Yanga wanapata ushindi katika mchezo wa leo Jumamosi dhidi ya Namungo FC, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amewataka wachezaji wa timu hiyo kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo kwa lengo la kubakia kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.
Yanga ambao kwa sasa wanakamata nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na pointi 57 nyuma ya vinara Simba wenye pointi 61, leo Jumamosi watacheza dhidi ya Namungo FC katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
Kocha huyo amesema kuwa anachokikata kutoka kwa wachezaji katika mchezo huo ni kuweza kupata ushindi kwa kuwa ndiyo lengo kuu katika mechi zao zote zilizobakia kwa sasa licha ya kutambua ugumu uliopo dhidi ya timu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka ndani ya benchi la timu hiyo ni kuwa tayari Nabi ameshatoa majukumu kwa wachezaji kuelekea katika mchezo huo na matokeo ambayo anayahitaji ili kuweza kujiweka katika wakati mzuri wa kupigania ubingwa.
“Kocha amewaambia wachezaji na amekuwa akiwasisitiza kwamba ushindi katika mchezo wa Jumamosi ni kitu muhimu kutokana na presha ambayo upande wetu kwa sasa lakini ugumu wa timu ambayo tunacheza nayo.
“Kitu kikubwa amewataka wapambane, wajue ukubwa na thamani yao hasa katika mechi hizi ambazo zimebakia na hata katika mazoezi ambayo yamekuwa yakifanyika huku Mtwara hilo ndiyo jambo amekuwa akilipigia kelele wakati wote,” alisema mtoa taarifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment