May 15, 2021


 SIMBA inatarajiwa kushuka uwanjani leo Jumamosi katika mchezo ambao inawezekana ukawa ni mwendelezo wa timu hiyo kuandika historia ya kipekee kama watafanikiwa kusonga mbele na kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Matumaini ya Simba kufanya vizuri msimu huu, yanakuja kwa kuwa kumekuwa na imani hiyo kutokana na mwendelezo wao mzuri katika michuano hiyo msimu huu tofauti na ilivyokuwa miaka mingine ya nyuma.


Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez, amefunguka kuwa, ana uhakika timu yake itapata matokeo dhidi ya Kaizer Chiefs kwenye mechi zote mbili za robo fainali.


Barbara amesema alikaa na kocha, wachezaji pamoja na benchi la ufundi la timu yake, akabaini kuwa kila mtu morali yake ipo juu, hivyo kuna kila sababu ya wao kupata ushindi kwenye mechi hizo.

 

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo kwa upande wa uongozi, Barbara alisema wameshamaliza kila kitu na wamewaambia wachezaji bonasi watakayopata kwa kushinda mchezo huo, hivyo hana wasiwasi kwa kuwa anajua wachezaji wake hawawezi kumuangusha.

 

“Naona kabisa tukishinda mechi zote mbili kwa uwezo wa Mungu, tutawafunga Kaizer hapa Afrika Kusini na tutakwenda kuwafunga pia kwenye uwanja wetu wa nyumbani pale kwa Mkapa


“Sisi kama viongozi tumeshacheza party yetu na wachezaji wanajua bonasi gani watapata kama watashinda hapa na nini watakivuna wakishinda Dar.

Huu ni mchezo muhimu kuliko michezo mingine yote waliyocheza msimu huu,” alisema Barbara.


Simba wanatarajia kushuka kwenye Uwanja wa Soccer City kutupa karata yao ya kwanza kwenye Hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic