May 20, 2021

 


MJUMBE wa Kamati ya Klabu ya Yanga katika masuala ya usajili, Injinia Hersi Said amesema kuwa huwa anavaa jezi ya Kaizer Chiefs pale anapokuwa na furaha.

Injinia ameongeza kuwa hiyo ilikuwa ni zawadi aliyopewa na mtoto wa mmiliki wa timu hiyo ya Afrika Kusini.

"Hii jezi ya Kaizer Chiefs nilipewa na mtoto wa mwenye timu katika siku ya maadhimisho ya timu hiyo ina historia nzuri kwangu ni ya miaka mingi imepita na hii jezi naivaa siku ambayo nikiwa na furaha,".

Jana Mei 19 wakati ubao wa Jamhuri, Dodoma ukisoma JKT Tanzania 0-2 Yanga injinia aliutinga uzi huo ikiwa ni ishara ya furaha kwake.

Pia kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika ujumbe mrefu kuelezea jezi hiyo ambapo alisema kuwa alipewa uzi huo mwaka 2020.

Jina la mtoto wa mmiliki wa timu hiyo ambayo alitoa mualiko kwa Yanga ulisimamiwa na Bobby Kaizer ambaye ni Meneja wa timu hiyo.

Ilikuwa ni katika sherehe ya kuazimisha miaka 50 ya timu hiyo ambapo na wao waliwakabidhi Kaizer Chiefs jezi ya Yanga yenye chapa ya GSM.

9 COMMENTS:

  1. Huu ni upuuzi wa hali ya juu. Wadanganye watoto wakubwa tunajua unafurahia kaizer chiefs kuofinga simba. Nilidhani utafirahia yanga kuifunga simba kumbe umeshakata tamaa hadi sasa unanunua furaha kutoka timu zingine? Mbona Al Ahly alipomfunga simba hukutinga red? Akili matope

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mazee umeandika huku unakimbizwa au ulivyoona hiyo jezi umepata kitete???��

      Delete
    2. Povu hahaahahaha! uhuru wa kuvaa chochote hata we vaa ya Mwadui au hata ya Mamelod

      Delete
  2. Utopolo wao unaanzia kwa viongozi wao

    ReplyDelete
  3. Safi sana endelea kuwavuruga nguruwe fc

    ReplyDelete
  4. Anamvuruga nani hiyo, kulikuwa na kipindi mnapokea wageni lakini haikuwadaidia sembuse kuvaa jezi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mmevurugwa balaa, jiandaeni kutoa kafara kama kawaida, kwanini safari hii msimtoe Haji Manara?

      Delete
  5. Tutakutoa wewe usiye na thamani, maana mechi yenyewe ngumu

    ReplyDelete
  6. Kama kiongozi hajitambui je anaowaongoza

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic