May 18, 2021


 HARRY Maguire nahodha wa kikosi cha Manchester United amejipa matumaini kuwa anaweza kuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza mchezo wa fainali ya Europa League.

Hivyo ikiwa hatakuwa fiti kwa muda uliobaki kuna hatihati atakosekana kwenye mchezo wa fainali ya Europa licha ya kuwa anahitaji kucheza.

Nyota huyo alipata maumivu ya kifundo cha mguu katika mchezo dhidi ya Aston Villa na alitakiwa kuwa nje kwa muda wa wiki mbili.

Kumekuwa na hofu kubwa kutoka kwa kocha wake Ole Gunnar Solskajer kuwa beki huyo anaweza kuikosa fainali dhidi ya Villarreal Jumatano ijayo. 

Kocha huyo amesema:"Nilipozungumza naye alionekana kuonyesha matumaini ya kurudi ila kwa sasa tunaelekeza nguvu uwanjani, tunaweza kumrejesha lakini sio mapema mpaka pale atakapokuwa fiti," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic