IMERIPOTIWA kuwa mabosi wa Tottenham wameziambia timu ambazo zinahitaji kupata saini ya mshambuliaji wao Harry Kane ziache mara moja kwa kuwa hesabu zao ni kwenye mechi zao za Ligi Kuu England ambazo ni za lala salama.
Taarifa zilieleza kuwa Jumatatu, Mei 17, Kane aliwaambia mabosi wake kuwa anahitaji kuuzwa msimu ujao ili kupata changamoto mpya jambo ambalo limekuwa likiwavuruga mabosi hao.
Timu ambazo zimekuwa zikitajwa kuhitaji saini ya nyota huyo kwa sasa ni pamoja na Manchester City inayonolewa na Kocha Mkuu Pep Guardiola, Manchester United inayonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunner Solkjaer pamoja na Chelsea ambazo zinashiriki Ligi Kuu England pia Barcelona na Real Madrid ambazo zinashiriki La Liga nazo zimekuwa zikitajwa kuwania saini ya nyota huyo.
Taarifa rasmi kutoka Klabu ya Spurs ilieleza kwa kifupi kujibu taarifa ya nyota Kane ambaye anahitaji kupata changamoto mpya ilieleza kuwa kwa sasa malengo yao na hesabu zao zote ni kwenye mechi zilizobaki kwa ajili ya kumalizia msimu wa Ligi Kuu England ambapo timu hiyo imebakiza mechi mbili.
"Mtazamo wetu mkubwa kwa sasa ni kwenye mechi ambazo zimebaki kwa ajili ya kumaliza msimu, mambo mengine hatuyatazami kwani hili suala kila mmoja anapaswa kuliangalia kwa umakini,".
0 COMMENTS:
Post a Comment