May 18, 2021


KOCHA mpya wa Mtibwa Sugar, Mohamed Badru leo Mei 18 ameanza kazi yake kwa timu yake kusepa na pointi tatu jumla mbele ya Mbeya City.

Katika mchezo wa leo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili, Mtibwa walicheza kwa utlivu huku Mbeya City wakiwa na mipago ya kushtukiza kusaka ushindi.

Ilibidi Mtibwa Sugar wasubiri mpaka dakika ya 11 kupachika bao la kuongoza kupitia kwa Kelvin Kongwe Sabato na lilidumu mpaka muda wa mapumziko.

Kipindi cha pili Mbeya City walijitahidi kusaka bao la kuweka mzani sawa ila milango ya Aboutwalib Mshery ilikuwa migumu na liliongezwa bao la pili kupitia kwa George Makang'a dakika ya 61 na pasi zote mtengeneza mipango alikuwa ni Salum Kihimbwa.

Mbeya City walipachika bao kipindi cha pili kupitia kwa Kibu Denis ila mwamuzi alinyanyua kibendera kwa ishara kwamba mfungaji alikuwa ameotea.

Unakuwa ni ushindi wa pili mfululizo kwa Mtibwa Sugar wakiwa Uwanja wa Jamhuri baada ya mchezo wao uliopita kushinda bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons na mtupiaji alikuwa ni Salum Kihimbwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic