UWEZO wa mchezaji kuwa bora ndani na nje ya uwanja unasimamiwa na juhudi isiyokuwa ya kawaida katika mazoezi huku msingi wa yote ukiwa unabebwa na nidhamu.
Wapo mastaa wengi Bongo ambao wana uwezo mkubwa ila kwenye upande wa nidhamu kwao imekuwa ni F jambo linalowafanya washindwe kutusua zaidi ama kuipa timu matokeo ambayo wanahitaji ila wakichukua hatua na kubadilika wana nafasi ya kufikia malengo yao.
Hawa hapa baadhi yao Spoti Xtra inakuletea:-
Jonas Mkude
Miongoni mwa makocha ambao amepita mikononi mwao na kukubali uwezo wake ni pamoja ni Masoud Djuma, Patrick Aussems na hata aliyebwaga manyanga hivi karibuni Sven Vandenbroeck bado alikuwa ni chaguo la kwanza kwake.
Desemba 28 alisimamishwa na uongozi wa Simba kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu. Habari zinaeleza wachezaji wenzake waliomba akae pembeni mechi 10 kwa kuwa alishindwa kuwasikiliza.
Yalitimia na mechi 10 alikosekana ikiwa ni pamoja na zile za Ligi ya Mabingwa Afrika chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes raia wa Ufaransa.
Mkude aliliambia Spoti Xtra kuwa bado yupo ndani ya ardhi ya Bongo huku akigoma kuzungumzia ishu yake ya kusimamishwa. Ila kwa sasa tayari amesharejea kikosini na ameanza kazi.
Reliats Lusajo
Mshambuliaji ndani ya kikosi cha KMC ambaye alikuwa shujaa ndani ya Klabu ya Namungo msimu wa 2019/20 na alihusika kwenye kuipandisha ligi msimu wa 2018/19 kwa sasa alipitia kipindi kigumu ndani ya KMC.
Alipokuwa KMC, Lusajo Januari 7, 2020 alisimamishwa na uongozi wa timu hiyo kwa kile kinachoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu.
Lusajo alianza kuingia kwenye mfumo wa KMC baada ya kuwa ni chaguo la kwanza ambapo kwenye upande wa kucheka na nyavu ndani ya Ligi Kuu Bara alitupia mabao manne mambo yalikuwa magumu KMC amerejea Namungo.
Bernard Morrison
Nyota huyu wa Simba mwenye ni ingizo jipya ndani ya kikosi hicho akitokea ndani ya kikosi cha Yanga amekuwa hana bahati linapokuja suala la nidhamu.
Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting wakati Simba ikifungwa bao 1-0 alikutana na rungu la Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kwa kosa lakuonekana akipigana na beki Juma Nyosso na alifungiwa kucheza mechi tatu.
Morrison anakumbukwa pia hata alipokuwa Yanga alikuwa ni mtu wa matukio yasiyo na nidhamu ambapo kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba, alipofanyiwa mabadiliko alitoka uwanjani mazima.
Ibrahim Ajibu
Maisha yake Simba kikosi cha kwanza yanasuasua ila amekuwa akitajwa kuwa miongoni mwa wachezaji ambao ni wachelewaji kambini.
Zama zile za Sven Vandenbroeck aliwahi kusimamishwa kwa muda kukitumikia kikosi hicho baada ya kuchelewa kuripoti kambini.Uwezo wa miguu yake unadondoshwa taratibu na nidhamu.
Juma Nyoso
Mkongwe huyu rekodi zake zinaonyesha kuwa ni miongoni mwa watu wa matukio yasiyo ya kiungwana ndani ya uwanja na nje ya uwanja.
Kwa msimu huu wa 2020/21 atakumbukwa kwa kitendo chake cha kurushiana ngumi na Bernard Morrison wa Simba, Uwanja wa Uhuru wakati timu yake ikishinda bao 1-0 dhidi ya Simba. Adhabu yake iliisha na sasa maisha yanaendelea.
Salum Kimenya
Kiraka huyu wa Tanzania Prisons anaingia kwenye orodha ya nyota wenye uwezo ila nidhamu bado kwa kuwa alimpiga mchezaji mwenzake ndani ya Uwanja wa Nelson Mandela wakati timu yake ikishinda bao 1-0 dhidi ya Simba.
Morrison ndiye aliyekutana na kibano kutoka kwa Kimenya ambaye kutokana na kosa hilo alifungiwa kutocheza mechi tatu na Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF). Adhabu yake iliisha na sasa maisha yanaendelea.
0 COMMENTS:
Post a Comment