KOCHA Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa anataka kumuona mshambuliaji wake Sergio Aguero anaonyesha kiwango cha juu uwanjani na anahitaji kumuona akicheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kiwango cha nyota huyo ndani ya kikosi cha City kimezidi kuporomoka kwa sasa jambo ambalo limekuwa likimfanya akose kujiamini.
Pia kwa sasa imekuwa ikielezwa kuwa Guardiola hana uhusiano mzuri na Aguero jambo ambalo limekuwa likimfanya awe anamuweka benchi.
Aguero msimu utakapomeguka anasepa mazima kwa kuwa mkataba wake unakwisha na timu ilitoa taarifa rasmi kwamba hataongeza mkataba.
Guardiola amesema:"Nafikiri kwenye mchezo dhidi ya Newcastle alikuwa hayupo fiti lakini hata sasa bado hajawa fiti asilimia 100, nafikiri atakuwa tayari kwa michezo kadhaa.
"Bado kuna michezo kadhaa na ninadhani nitafanya maamuzi magumu katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya Chelsea nafikiri anaweza kucheza,".
0 COMMENTS:
Post a Comment