BAADA ya kupewa mapumziko ya siku nane
kikosi cha Polisi Tanzania kimeingia kambini
kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu
Bara dhidi ya Simba.
Polisi wanatarajia kuwakaribisha Simba Juni 19,
mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza.
Wachezaji wa timu hiyo walipewa mapumziko
baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi dhidi
ya Coastal Union ambapo Polisi iliibuka na
ushindi wa bao 1-0.
Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Hassan Juma alisema
kuwa: “Timu ilianza mazoezi mapema wiki hii
kwenye Uwanja wa TPC, Moshi kwa ajili ya
kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Simba.
“Askari wa mwamvuli wamerejea wakiwa na ari
na morali ya kupambana ya kuhakikisha
malengo ya timu kwa msimu huu ya kukusanya
pointi 12 katika michezo iliyobaki ukiwemo ule
wa Simba yanaweza kufikiwa.”
Polisi Tanzania imebakiwa na michezo minne
kuelekea mwishoni mwa msimu huu, ikiwa ni
dhidi ya Simba, Kagera Sugar, Mwadui na Ruvu
Shooting, na ipo katika nafasi ya sita kwenye
msimamo ikiwa na pointi 41.
Polisi tz najua inatumia uwanja ulioko moshi... KuKulikoni mwanza na hamtuambii hata sabaabu
ReplyDelete