KWA mara ya kwanza, Kocha Mkuu wa Simba,
raia wa Ufaransa, Didier Gomes Da Rosa,
ametoa kauli ya kuonyesha wazi kuvutiwa na
uchezaji wa kiungo mshambuliaji wa Dodoma
jiji, Dickson Ambundo.
Juzi Jumatano, Gomes alikiongoza kikosi chake
kwenye mchezo wa robo fainali ya michuano ya
Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC),
ambapo Simba ilifanikiwa kutinga hatua ya
nusu fainali ya michuano hiyo, baada ya
kuibuka na ushindi mbele ya Dodoma Jiji mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.
Akizungumza na Championi Ijumaa baada ya
mchezo huo kumalizika, Gomes alikishukuru
kikosi chake kwa kufanikisha malengo yake ya
kuingia hatua ya nusu fainali, lakini
aliwapongeza Dodoma Jiji kwa mchezo mzuri
huku akikiri wazi kuvutiwa na uchezaji wa
Ambundo.
“Mchezo wetu haukuwa rahisi kama wengi
wanavyodhania baada ya kupata ushindi,
kimsingi niwapongeze wachezaji wangu kwa
kufikia lengo la kuingia hatua hii, ila pia
niwapongeze wapinzani wetu Dodoma Jiji kwa
mchezo mzuri, ila nimevutiwa zaidi na kiungo
wao mshambuliaji Ambundo.
“Uchezaji wa kiungo huyo, unaonyesha kujua
zaidi majukumu yake uwanjani na ndiyo maana
utaona alitusumbua kiasi cha kunifanya nifikirie
kwa umakini namna ya kumdhibiti na ndiyo
maana niliingiza viungo kama Erasto Nyoni,
Mzamiru Yassin na Thadeo Lwanga,” alisema
Gomes.
Hongera ambundo
ReplyDeleteHuyo keshakuwa wa Mnyama wala asijaribu yeyote kujaribu kukata mbele kujivuwa na kikumbo
ReplyDeleteMnyama tayari huyu
ReplyDelete