POZI la Kocha Mkuu wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Gavin Hunt alipokuwa kwenye benchi la ufundi jana Mei 15 wakati timu yake ikishinda mchezo wa kwanza mbele ya Simba limezua gumzo kwa wadau wa mpira kutokana na namna ambavyo alifanya huku kila mmoja akitoa maoni yake.
Wapo ambao walisema kuwa hicho ni kicheko cha furaha na wengine wakisema kuwa ni kicheko cha mshangao wa idadi ya mabao aliyoshinda.
Alifanya hivi aliposhuhudia bao la nne kwa timu yake ya Kaizer Chiefs lililopachikwa na Leonardo Castro na ubao wa FNB ulisoma Kaizer Chiefs 4-0 Simba.
Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ilipoteza mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ina kazi ya kupindua meza katika mchezo wa pili, Uwanja wa Mkapa, Mei 22 ili kuweza kusonga mbele hatua ya nusu fainali.
Najua hapo waandishi wa hii blog mlivyo vilaza mtakuwa mmefurahia
ReplyDeleteYaani ndio wameona habari muhimi , wanapenda habari za kimbeyambeya
DeleteHahaha aiseee jamani hilo pozi ni la dharau sana
ReplyDeleteTimu ipo nafasi ya 9 haiwezi isumbua timu ya nafasi ya kwanza kwenye ligi ya tz
ReplyDeleteEti nyie hivi 4-0 ndiyo 4G?
ReplyDeleteHivi ile Simba ya kucheza na Bayern au Barcelona ndiyo ile iliyocheza jana au walipeleja Simba Queens?
ReplyDeleteMimi naona nafasi ya kucheza dhidi ya Kaizer Chiefs wangeipata akina wale jamaa waliotoka droo na Namungo wangeona hao akina Kaizer cha mtema kuni
ReplyDeleteAssist bora so far katika mashindano haya ni ya Zimbwe jana
ReplyDeleteJumamosi atakuwa mwekundu Kama kaingizwa kwenye tanuli
ReplyDeleteMaana ya mpira unadunda utasikia tarehe 22 kama tumefunga 4 basi wap watafungwa 5 watu hawaamini lakini ndoo ukweli na hauna kificho dunia itasimama
ReplyDelete