MSHAMBULIAJI wa Yanga FC, Fiston Abdoul Razack raia wa Burundi ameibuka na kusema kuwa hatamani kubaki tena ndani ya kikosi cha timu hiyo baada ya kocha Cedrik Kaze kuondoka.
Mrundi huyu aliyetua Yanga katika usajili wa dirisha dogo msimu huu na kusaini kandarasi ya miezi sita, amefanikiwa kufunga mabao mawili tu, moja kwenye Ligi Kuu Bara na lingine katika Kombe la FA.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Fiston alisema kuwa: “Kwa sasa Yanga hawajanifuata kuhusu kuongeza mkataba na wala sitamani kuongeza tena mkataba.
“Najua kuwa wananchi walitamani kuona makubwa kutoka kwangu na mengi ila mimi kuna kitu nimekiona kwenye hii timu yaani wana tabia ya kuonjeshana (kukupa nafasi finyu uwanjani) tu hawawezi kumuacha mtu azoee.
“Mtu asipofunga kipindi cha kwanza kipindi cha pili wanawaza kumtoa na usipofunga mechi moja basi mechi ijayo hupati nafasi ya kuanza.
“Kama kocha Cedric Kaze angekuwepo basi ningefanya makubwa zaidi maana yule ananijua na anajua jinsi ya kunitumia.”
Pumbavu!!! Mlikuwa mnaleta ubaguzi kama kawaida yenu wakati uwezo ni wa kawaida tu
ReplyDeleteHatukuhitaji maana hakuna jipya tuliloliona zaidi ya nyodo na dharau kwa wazawa
Aondoke tu la sivyo tutamwondoa, garasa tu
ReplyDeleteWaondoke hata yule wa Abgola sisi hatujali na wataibakia watatuia ubingwa tena wa msimu huu
ReplyDeleteMwandishi ongeza umakini. Yanga FC ni kitu gani hichoππ
ReplyDeleteMwandishi ongeza umakini. Yanga FC ni kitu gani hicho ππ
ReplyDelete