May 17, 2021

 


BAADA ya ubao wa FNB Soccer City Mei 15 kusoma Kaizer Chiefs 4-0 Simba, wawakilishi wa Tanzania wameweka wazi kwamba watapindua meza kibabe Uwanja wa Mkapa.

Huo ulikuwa ni mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika ulimfanya Kocha Mkuu wa Simba, Dider Gomes kushuhudia idadi kubwa ya mabao akiwa kwenye benchi kwa mara ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Leo kikosi kinatarajiwa kuwasili ardhi ya Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na ule wa marudiano dhidi ya Kaizer Chiefs.

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 22 ambapo Simba wameweka wazi kwamba wanaimani ya kupata matokeo chanya ili kuweza kusonga mbele.

Gomes amesema:"Bado tuna muda mwingine kwa ajili ya kupata matokeo na muhimu kwetu kuwa bora zaidi ili kuweza kushinda," .

Katika mchezo ujao Simba ili iweze kutinga hatua ya nusu fainali inakazi ya kusaka ushindi wa mabao matano huku ikilinda lango lake lisitikiswe na wapinzani hao ambao wana kasi ya kucheka na nyavu na mpango wao ni wa kushambulia kwa kushtukiza.

5 COMMENTS:

  1. Weeeeee thubutu! Hata benchi hampindui

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nyie ndo mnaozimiaga kwa sababu Mpira wenyewe mmeanza kushabikia Instagram ndio shida

      Delete
  2. Kupania kupindua meza ni jambo zuri,lakini kwa tuliotazama mpira ule,hakika ni ngumu labda tusubir maajabu mengine katika soka letu.

    ReplyDelete
  3. Suala sio kupanga au kutopanga, suala hapo ni Uwezo, wachezaji wengi wangependa wapindue meza lkn waliokua kwenye mechi ile wanajuaghuhuli yake,
    Kwa mashabiki wanaweza kupindua meza lkn wachezaji wanajua ugumu wake

    ReplyDelete
  4. Ki ukweli mabeki wa Kati siku hiyo walikuwa hivyo na haikutakiwa beki za pembeni kupanda Huku na beki za Kati Zina panda Simba sc hawajatutendea haki

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic