May 14, 2021


WAKATI Kaizer Chiefs Jumatano ilipokubali kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 katika mechi ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini dhidi ya Moroka Swallows, Simba walikuwa macho kuufuatilia mchezo huo kwa lengo la kuzinasa mbinu za wapinzani wao hao.

 

Uamuzi wa Simba kufanya hivyo umekuja ikiwa ni kuelekea mchezo wao wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Jumamosi hii.

 

Kaizer Chiefs na Simba, zinatarajiwa kupambana kwenye Uwanja wa FNB uliopo Johannesburg, Afrika Kusini, kisha marudiano ni Mei 22, mwaka huu Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Kwa sasa Simba tayari ipo nchini Afrika Kusini ikiendelea na maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo wa Jumamosi.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola, alisema kuwa wanawatazama wapinzani wao kwa ukaribu ili kujua namna ya kuwakabili kwa kuwa wanahitaji matokeo mazuri.

 

“Kiukweli bado tunaendelea kuwafuatilia wapinzani wetu kwani ni timu nzuri na ina wachezaji ambao wanaleta ushindani, kabla ya hapo tuliangalia mechi zao zilizopita na bado tunawafuatilia ili kujua namna gani wanafanya ndani ya uwanja.


“Kuna mechi ambayo wanacheza hivi karibuni, pia tunawafuatilia kisha tutajua namna gani tunaweza kupata ushindi dhidi yao. Kikubwa ni kwamba Watanzania waendelee kutuombea kwani ushindani ni mkubwa,” alisema Matola.

 

TIZI LAO


Simba baada ya kufika Afrika Kusini walifanya mazoezi kwenye Viwanja vya Discovery Soccer Park – Sandton.Taarifa kutoka kambini huko Afrika Kusini, zinasema kwamba, katika mazoezi hayo ya awali, Kocha Gomes alianza taratibu ili kurudisha hali ya utimamu na kuondoa uchovu wa safari kwa wachezaji, kabla ya kuanza kufanya mazoezi ya mbinu kwa nguvu.

 


2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic