May 14, 2021

 

KOCHA wa zamani wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems, amefunguka kuwa ubora wa timu hiyo kwa sasa umekuwa mkubwa kutokana na kusajili wachezaji wenye uwezo wa kutumikia timu hiyo huku akisisitiza hatashangaa ikiwa Simba itafanikiwa kuifunga Kaizer Chiefs, kesho Jumamosi katika mchezo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Aussems ametoa kauli hiyo kuelekea katika mchezo huo ambao unatarajiwa kupigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Soccer City uliopo Afrika Kusini. 

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Aussems alisema kuwa kufanya vizuri kwa Simba kunatokana na ubora wa usajili uliofanywa na timu hiyo, hivyo ina kila sababu ya kupata matokeo katika mchezo wowote wa Ligi ya Mabingwa Afrika. 

 

“Kwanza mchezo wao na Kaizer hautakuwa rahisi licha ya Kaizer kutopewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kutokana na namna timu ilivyo kwa sasa, lakini bado mchezo utakuwa mgumu kwa sababu wanavyocheza kwenye Ligi ya Mabingwa wanakuwa tofauti zaidi.

 

“Lakini bado imani yangu kubwa ipo kwa Simba, hili linatokana na namna walivyofanikiwa katika usajili wa timu kwa kuweza kuongeza wachezaji wenye uwezo wa kupambana na ndiyo kitu pekee kitakachoweza kuibeba kupata matokeo katika mchezo huo,” alisema Aussems.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic