MBINU za Didier Gomes, Kocha Mkuu wa Simba akisaidiana na Kocha Msaidizi Seleman Matola leo Mei 15 zimegonga mwamba mbele ya wapinzani wao Kaizer Chiefs katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fanali ya kwanza kwa kukubali kichapo cha mabao 4-0.
Ni Eric Mathoto dakika ya 6 alipachika bao la kwanza kwa kichwa akiwa ndani ya 18 baada ya mabeki wa Simba kushindwa kuweka ulinzi imara kwenye eneo lao la 18 na Samir Nurkovic ambaye alikuwa mwiba leo kwa Simba alipachika bao la pili dakika ya 34 na kuwafanya Simba waende mapumziko wakiwa na mzigo wa mabao mawili.
Ngoma iliendelea kupigwa kwa kasi huku Kaizer Chiefs wakicheza kwa kushambulia kwa kushtukiza huku Simba wakiwa kwenye umiliki na kushindwa kumalizia nafasi wanazotengeneza.
Dakika ya 57 chuma cha tatu kilipachikwa na yuleyule aliyewafunga kipindi cha kwanza Nurkovic kwa makosa yaleyale ya mabeki.
Kabla ya mpira kukamilika ni Castro Leonardo Casro ambaye alipachika msumari wa mwisho na kuivunja rekodi ya kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula kuokota mabao mawili pekee kwenye mechi tano ambazo alicheza hatua ya makundi.
Jitihada za Chris Mugalu, Clatous Chama, Luis Miquissone ziligonga mwamba na kufanya timu icheze bila kuwa kwenye hali ya kuleta hatari kwa wapinzani.
Sasa kazi inabaki Mei 22 kwa Simba kusaka ushindi wa mabao matano bila kuruhusu kufungwa ili waweze kutinga hatua ya nusu fainali.
Pole sana mtani ndio ukubwa huo ila usikate tamaa maana nafasi bado unayo kwani bado una dakika tisini za marudiano na kawaida yako mtani kwa Mkapa hatoki mtu au sio mtani
ReplyDeleteWewe kweli ni mtu mstaarabu sana.
DeleteHao kabla ya kuikejeli Simba kwanza walie kutokana na hali isiyotabirika ya timu yao. Makocha wamebadilishwa kila mwezi, ahadi ya mamilioni kwa mastaa ikipatikana ushindi, yote hayo hata kuleta tija. Mastaa na makocha ambao waliokuwa mwiba na kujikuta hamna kitu baada ya kujiunga nao. Na sasa wangojee aibu nyengine baada Namungo na huku ubingwa ikiwa ndoto
ReplyDeleteTatizo kikosi chetu kilishindwa kuwaheshimu kaiser chief ndo maana tukafungwa nyingi
ReplyDeleteTatizo bekibwa simba hawachezi mipira juu ,na manula mfupi na washambuliji wa ship warefu na hodari kwa mipira ya vichwa gamu hii na ile ya sudan sawa sawa kule bahati simba golini alikuwa kakolanya mrefu kaokoa jahazi kiufupi tizameni game zote hata za ligi utakuta simba wanafungwa kwa mipira ya juu ya vishwa time yeyote ile ikiwa ina washezaji wa kufunga kwa vichwa basi simba watalala hili tatizo lipo na wanalijuwa na halikufanyiwa kazi pili wawa anafata mipira hakabi mtu hilo tatizo mabeki wote simba hawawezi mipira ya juu pili kocha alifanya kosa kubwa kuamini kuwa atacheza vile alipokuwa tayari 2 alikuwa afanye mabadiliko aingize defence na manula atoke aingie kakolanya lakini alishindwa akaitoa morali ya time na gemu inayo fuata wakieka kikosi hicho hicho pia watafungwa game inayo fuata simba wacheze mpira wa machuti hapo watashinda lakini wakijaribu kuingia kati watashindwa game inayo fuata wamtie ndemla apige mashuti wavamie hapo wanaweza kushinda ,pili kukaa week tatu bila ya meshi pia iliondoa fitness ya timu inawezeka simba wakapindua wakijiamini anything possible
ReplyDeleteMlima wa kufunga Goli tano(5) kwa team bora si mchezo
ReplyDeleteSimba wanacheza pira pilau pira biriani sasa unataka wacheze mpira gani
ReplyDeleteSisi mashabiki wa nguruwe fc tutashinda, hata tusiposhinda magoli bora tushinde njaa
ReplyDeleteHivi nyie eti 4-0 ndiyo 4G?
ReplyDeleteTatizo la Simba ni Manula na Tshabalala,wadau washawahi sema watafutiwe wabadala lakini sifa za uongo wanazopewa ndiyo results zake,Tshabalala alitoa pass mbili za magoli,Manula alifungwa goli la 2 kizembe kabisa.Simba wakiendelea kuwakumbatia ipo siku watakula Saba.Naungana na mdau mmoja hapo juu kwamba baada ya 2 ilitakiwa aingize Nyoni na Kennedy juma angecheza upande wa Tshabalala,kwanza ni mrefu halafu ana nguvu.Mchezo wa marudiano tutapigwa Tena Taifa coach asipokuwa makini na upande wa Tshabalala,acheze Kennedy Juma.Tusubiri tuone na mpira was pass nyingi hatutaweza kushinda hata kwa dawa,inabidi tupige mashuti hata nje ya 18
ReplyDelete