AZAM FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uiochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Ni Prince Dube alifungua pazia la ushindi dakika ya 11 kwa kupachka bao ambalo liliwekwa usawa na nyota wa KMC Abdul Hilary dakika ya 41.
Wakati KMC wakiamini kwamba ngoma imekamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 na kupata pointi moja ngoma ilipinduka dakika ya 90+2.
Nahodha wa Azam FC, Agrey Moris alipachika bao la ushindi na kuwafanya wasepe na pointi tatu mazima.
Dube anakuwa ni namba moja kwa kutupia akiwa na mabao 13 ndani ya Ligi Kuu Bara huku timu yake ikifikisha jumla ya pointi 57 nafasi ya tatu.
Safi
ReplyDelete