May 21, 2021


 NAHODHA msaidizi wa kikosi cha Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema kuwa licha ya timu hiyo kuwa na matokeo yasiyotabirika katika michezo ya hivi karibuni, bado hawajakata tamaa katika malengo yao ya kutwaa ubingwa msimu huu.


Yanga,Jumatano waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania na kufikisha pointi 61, hivyo kuwafikia vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara, Simba ambao wamejikusanyia pointi 61 licha ya kuwa na michezo minne pungufu dhidi ya Yanga.

 

Yanga wamekuwa na mwenendo wa kusuasua ambapo katika michezo nane mfululizo iliyopita wamefanikiwa kushinda michezo mitatu pekee, wamepoteza miwili na kutoa sare kwenye tatu.


Matokeo hayo yameonekana kuzidi kuwapunguza kasi Yanga katika vita ya kuwania ubingwa wa msimu huu.

 

Akizungumzia mipango yao Mwamnyeto alisema: “Ni kweli tumekuwa na mwendo wa kusuasua kwenye michezo yetu iliyopita, lakini tunaamini kuwa hiyo ni hali ya kawaida na ni suala ambalo tayari linafanyiwa kazi na benchi letu la ufundi.

 

"Hivyo, tunapambana kuhakikisha tunafikia malengo yetu msimu huu ikiwemo kumaliza katika nafasi za juu, na hata kutwaa ubingwa.”


Naye Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli akizungumza na Championi Ijumaa, alisema:

 

“Tunaendelea kujenga kikosi chetu, lakini pia tunaendelea kupigania malengo yetu ya kutwaa ubingwa msimu huu, changamoto ya matokeo ni kitu cha kawaida na hatuwezi kukata tamaa.”



6 COMMENTS:

  1. Ubingwa upi? Kama ni ligi kuu bara msahau.... Mjaribu nxt time

    ReplyDelete
  2. Unajuwa hawa jamaa inabidi waonewe huruma wanautanani sana kwakuwa wanausikia kwa masikio tu tangu miaka mine iliyopita na juu ya hilo nasikia mganga wao kutoka Pemba kasisitiza sana kujipa tamaa baada ya kupokea chake

    ReplyDelete
  3. Nawashauri uto wajipange kwa msimu ujao,lakini Kama wanafikria msimu huu wataumiza vichwa bure.

    ReplyDelete
  4. umeongea kweri lakini itawezekana

    ReplyDelete
  5. Ubingwaa waa straikaa anagoli 7, boraaa yulee mkongo alimalizaa na 12

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic