May 9, 2021

MEI 8, 2021 ilibidi uchezwe mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga, ila Yanga waligomea mabadiliko ya muda uliofanywa kabla ya mchezo huo ambao awali ulipangwa kuchezwa saa 11:00 Uwanja wa Mkapa ila Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) lilieleza kuwa utachezwa saa 1:00. Tazama namna Yanga walivyoondoka kwa kutumia mlango wa chumba cha mikutano ya Waandishi wa Habari.

 

12 COMMENTS:

  1. Walitoka ndukii kwa mlango wa uwani.Kwa kikosi kile ukitia timu hujipendi Katika watu walioshukuru jana ni kocha wa Yanga sahizi angekuwa Airport.Na kwa vile amekuja na mfuko wa plastiki ingekuwa safari rahisi.

    ReplyDelete
  2. Mimi nadhani wewe umeathirika akili Kama alivyo Manara wakati huu ni majira hapana jua Kali mbona unaweweseka?

    ReplyDelete
  3. Mchezo huu ulianzia February,wakundu wakakimbia,mnatafuta mnvua wakati imeisha

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unaumwa wewe! Mnyama akukimbie wewe wakati anakuwakilisha vyema kimataifa

      Delete
    2. Utopolo wamepata upenyo wacha watoke nduki, mbio sio za nchi hii... Ila mechi itapigwa na mtapasuka nyingi tu

      Delete
  4. Hahahaa kumbe walitokea mlango wa uani, wangefunga milango yote wasikimbie.... Wametia aibu Sana

    ReplyDelete
  5. Wakati huu ni majira ndio nini Utopolo. Ukiona timu inashangilia kususa jua mpira umewashinda.Kuna mwingine anamuota Manji!!! Ingizeni timu muone. Jana walikubali walipompigia mganga akawa shauri tokeni ndukii mkiingiza timu 5.Hersi alitaka wachezr kidogo wamuuwe.

    ReplyDelete
  6. Yaani mpaka mapovu zinawatoka?si mlisema simba hii level nyingine, mbona mnateseka?

    ReplyDelete
  7. Hivi Yanga ndio wanapanga ratiba?Sio Bodi ya Ligi na TFF?Mechi ikisogezwa mbele ni timu ndio zinasogeza mbele au mamlaka zinazohusika.Mechi ya kwanza kati ya timu hizi mbili ilipoarishwa nani alipanga tarehe ya jana?Ni Yanga?Wao wana mamlaka gani ya kutofuata ratiba iliyopangwa na kupanguliwa.Huwa wanashiriki kupanga ratiba??

    ReplyDelete
  8. wameogopa kutokea mlango mkubwa wanaweza kuta umefungwa duuu aibu kubwa

    ReplyDelete
  9. Hawa jamaa hawakufikiria faida au hasara kutokana na kuingia mitini, sasa ndio wansfikiri mambo yamekeisha. Hatuwa Zitachukuliwa na mechi itachezwa tena baadae lakini wajuwe kitendo walichokifanya cha aibu ni cha namna yake ambacho hakijatokea na sasa wangojee matokeo yake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic