May 14, 2021


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa wanatambua kwamba wapinzani wao Namungo ni timu imara ila watapambana kupata ushindi.

Kesho Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu kwenye mchezo wa ligi utakaochezwa Uwanja wa Majaliwa.

Walipokutana Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 1-1 Namungo na Bigirimana Blaise alikosa penalti baada ya Metacha Mnata kuokoa penalti hiyo.

Hassan Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa ni mchezo mgumu kwao kwa kuwa wapinzani wao pia ni timu imara ila hawatakubali kukosa ushindi.

"Ni wapinzani wazuri na tunatambua uimara wao, haina maana kwamba kupata nao sare wakati uliopita na sasa itakuwa hivyo hapana tupo tayari.

"Kikubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo kwenye mchezo wetu ujao na kila kitu kipo sawa mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti," amesema.

Kwa upande wa Namungo, Kocha Mkuu, Hemed Morocco amesema kuwa watapambana kupata pointi tatu. 

Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo na ina pointi 57 huku Namungo ikiwa nafasi ya 10 na pointi 35.

Kikosi hicho kwa sasa kipo Mkoani Lindi kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa majira ya saa 10:00 jioni na nyota wao Tuisila Kisinda ni miongoni mwa wale ambao wapo kwenye msafara huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic