HARUNA Niyonzima, kiungo mchezashaji wa Yanga amesema kuwa mchezo wa leo dhidi ya Simba unahitaji utulivu mkubwa kwa kila mchezaji ili aweze kufanya vizuri.
Yanga inaingia Uwanja wa Mkapa leo kusaka pointi tatu mbele ya Simba katika mchezo wa mzunguko wa pili ambao utachezwa Uwanja wa Mkapa majira ya saa 11:00 jioni.
Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, dakika 90 zilikamilika kwa timu zote mbili kutoshana nguvu na kugawana pointi mojamoja baada ya ubao kusoma Yanga 1-1 Simba.
Niyonzima amesema:"Mchezo wa Kariakoo Dabi ni mkubwa na ushindani ni mkubwa ila unahitaji utulivu mkubwa ili timu kupata ushindi hilo lipo wazi.
"Wapinzani wetu wanahitaji pointi tatu nasi pia tunahitaji mchezo hivyo yule ambaye amejiaandaa vizuri ndiye ambaye atashinda mchezo wetu," .
0 COMMENTS:
Post a Comment