KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu Nassreddine Nabi leo Mei 18 kimeanza safari kuelekea Dodoma kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kesho Mei 19, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma majira ya saa 10:00 jioni.
Baadhi ya wachezaji ambao wapo kwenye msafara huo ni pamoja na Feisal Salum, Bakari Mwamnyeto, Ramadhan Kabwili, Zawad Mauya na Metacha Mnata.
Mchezo wao wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, Yanga ilisepa na pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0.
Hivyo mchezo ujao utakuwa na ushindani kwa timu zote mbili ambapo JKT Tanzania watahitaji kulipa kisasi na Yanga wao watahitaji kulinda rekodi zao.
Kwenye msimamo wa ligi, Yanga ipo nafasi ya pili na pointi zake kibindoni ni 58 inawafuata JKT Tanzania walio nafasi ya 13 na pointi 33.
Mrudisheni Mhilu achukue nafasi ya Sarpong
ReplyDeleteKwani Saprong hayupo keshatimuliwa?
ReplyDelete