BAADA ya kukosekana kwenye michezo mitatu iliyopita ya Simba, beki wa klabu hiyo Joash Onyango amelazimika kupewa programu maalum, ili kuhakikisha anarejea akiwa kwenye kiwango bora.
Onyango na Lwanga walipata ajari mbaya ya kugongana vichwa katika mchezo wa robo fainali ya pili kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Mei 22, mwaka huu na kushindwa kuendelea na mchezo huo.
Katika tukio hilo Onyango alipata mpasuko mdogo kwenye paji lake la uso, na kupatiwa matibabu ambayo yamemfanya akose michezo mitatu mfululizo ya Simba, dhidi ya Dodoma Jiji, Namungo na mchezo wa jana dhidi ya Ruvu Shooting.
Akizungumzia maendeleo ya beki huyo kocha wa viungo wa klabu ya Simba, Adel Zrane amesema: “Onyango tayari alianza mazoezi lakini amelazimika kuendelea kukosekana katika kikosi chetu kutokana na kupewa muda wa kuponyesha majeraha madogo aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs.
“Benchi la ufundi tayari limempatia programu maalum ya kurudisha kasi yake pale
atakaporejea uwanjani, na kwa sasa yuko fiti kwa asilimia kubwa.”
0 COMMENTS:
Post a Comment