UONGOZI wa Ruvu Shooting umeweka wazi kwamba utapambana kupata matokeo chanya kwenye mechi zao ambazo zimebaki kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara.
Jana, Juni 3, ubao wa Uwanja wa CCM Kirumba ulisoma Ruvu Shooting 0-3 Simba na katika mchezo huo nyota wao wawili ambao ni Juma Nyosso ambaye ni beki na kipa wao namba moja alionyeshwa walionyeshwa kadi nyekundu.
Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa wapo imara licha ya kushindwa kupata matokeo mbele ya Simba watapambana katika mechi zao zijazo.
"Bado tupo imara na tuna mechi mkononi ambazo hizo zitatufanya tupate matokeo na kuwa katika sehemu salama.
"Wale ambao wanafikiria kwamba tutakuwa kwenye mwendo mbaya hao ni mawazo yao ila sisi tupo vizuri na tuna amini kwamba tutafanya vizuri ndani ya ligi mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema.
Kwenye msimamo wa ligi, Ruvu Shooting ipo nafasi ya 10 ina pointi 37 baada ya kucheza mechi 30 namba moja ni Simba ana pointi 67 baada ya kucheza jumla ya mechi 227.
0 COMMENTS:
Post a Comment